GETI LA DSJ LAPOTEZA MVUTO
![]() |
GETI LA DAR ES SALLAAM SCHOOL OF JOURNALISM(DSJ) LILILOPOTEZA MVUTO |
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari cha Dar es salaam school journalism DSJ walalamikia geti la kuingialia chuoni hapo kutokana na geti hilo kupoteza mvuto .
Akizungumzia swala hilo mmoja wa wanafunzi chuoni hapo Bi, Sayuni Richard amesema kuwa"Kwa geti la chuo halilizishi kwasababu huwezi kujua kama ni geti la chuo,pia nembo haiyonekani vizuri"
Pia Mwanafunzi huyo ameongezea kea kusema" Namuomba Mkuu wa chuo alitengeneze geti vizuri na kuliwekea nembo ili liwe na mvuto".
Vilevile mwanafunzi wa chuo hicho Bwana, Elick Ruben amesema kuwa"Yeye binafsi halizishwi na geti la chuo kwasababu mlinzi anatumia nguvu kubwa wakati wa kulifungua"
Pia mwanafunzi huyo ameongezea kwa kusema kuwa "anaomba geti hilo liboreshwe ikiwezekana waweke lile la mataili".
Comments
Post a Comment